Thursday, May 9, 2013

Ushauri Wa Naibu Waziri, Mheshimiwa January Makamba Kwa Vijana wakati wa Kufunga GIST Boot Camp

DSC01643

Mheshimiwa Naibu waziri idara ya Mawasiliano, Sayansi na teknologia, Mbunge wa Bumbuli Bwana January Makamba akifunga kambi ya wajasiriamali katika tekinologia ya Mawasiliano, aliwashauri vijana kutumia fursa za sasa vizuri vilevile akiyaasa makampuni makubwa nchini kuwekeza kwa vijana ambao wanaleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo katika Teknologia.
katika kambi hii GIST ilifadhiliwa na serikari ya Marekani na Finland kupitia InfoDev, LIONS@AFRICA, Benki ya Dunia , Nokia na Microsoft.
Vijana walipata Mafunzo, ushauri pia na kupata nafasi ya kuwasilisha biashara zao na miradi yao kwa wawekezaji, ambapo kijana wa Kitanzania Arnold Minde uwasilishaji wake na huduma aliyobuni kwa njia ya teknologia itakavyorahisisha namna ya ukataji wa tiketi za mabasi ya kwenda mikoani na uendeshaji wake kupitia Safariyetu.com
Vijana wetu wanatakiwa kujifunza namna ya kuwasilisha miradi yao mbele ya wawekezaji sawasawa, kujiandaa vilivyo n.k. GIST Boot Camp ilihusisha vijana mbalimbali kutoka Africa ya Mashariki na hivyo kuwepo na ushindani mkubwa wa mawazo, miradi na uwasilishaji wake kwa dakina tatu mbele ya wawekezaji hao.
DSC01338

DSC01330

DSC01246

DSC01244
DSC01244

No comments:

Post a Comment