Thursday, April 25, 2013

Baghdad, kenya, Pakistani na Wahindi Wauziwa vifaa feki vya kuchunguzia Mabomu


Mfanyabiashara wa kiingereza James McCormick amepatikana na hatia ya kuuza vifaa vya kuokotea mipira ya gofu ambao kila mpira unagharimu dola ishirini za kimarekani na akuzia taasisi za kijeshi katika nchi zenye migogoro ya kivita kwa dola elfu arobaini kwa kila kimoja. Mfanyabiashara huyu ameweza kujizolea Dola milioni sabini na tano katika nchi ya iraki pekee, mahakama ilieleza.Bwana James McCormick mwenye miaka 57 ambaye ni polisi wa zamani, amepatikana na kosa la udanganyifu kwa kuuza vifaa hivyo vya kuokotea mipira ya gofu kama vifaa vya kuchunguzia mabomu katika nchi mbalimbali ambapo kuna vita na watu wengi wanakufa.ameachiwa kwa dhamana na hukumu ya kesi yake itatolewa tarehe 2 mwezi wa tano.Faida kubwa ameipta kwenye vita la iraki ambayo watu wengi wamekufana uharibifu mkubwa.
http://www.lightwaysolutiontz.com/baghdad-kenya-pakistani-na-wahindi-wauziwa-vifaa-feki-vya-kuchunguzia-mabomu/

No comments:

Post a Comment