Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles MsondeNaibu Katibu
Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde UFAULU katika mitihani ya Taifa ya
kidato cha sita uliofanyika Februari mwaka huu umeongezeka
ikilinganishwa na wa mwaka jana. Hayo yamebainika baada ya Baraza la
Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo hayo likionesha kuwa
wanafunzi 44,366 sawa na asilimia 87.85 kati ya 50,579 waliofanya
mitihani hiyo wamefaulu huku 2,604 wakipata daraja sifuri. Kati ya
waliofaulu, wasichana ni 14, 622 na wavulana 29,744. Kulingana na
matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Naibu Katibu Mtendaji wa Necta, Dk
Charles Msonde, shule ya wasichana ya Marian ya Pwani imeongoza kitaifa
huku shule za Green Acres, Mzizima na St Maryâ zote za Dar es Salaam
zikiwa kwenye shule 10 za mwisho kitaifa. Akizungumzia matokeo hayo, Dk
Msonde alisema mwaka huu ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.20
ukilinganishwa na wa mwaka jana ambapo wanafunzi 46,658 sawa na asilimia
87.65 walifaulu huku mwaka 2011 waliofaulu wakiwa ni asilimia 87.24.
Alisema watahiniwa wa shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92,
wa kujitegemea 4,124 sawa na asilimia 53.87 ambao imeonekana
hawakufanya vizuri ikilinganishwa na wa mwaka jana ambapo waliofaulu
walikuwa ni asilimia 64.96. Aliongeza kuwa jumla ya watahiniwa 52,513
walijiandikisha kufanya mitihani hiyo na kati yao watahiniwa 50,611 sawa
na asilimia 96.38 walifanya huku 1,902 sawa na asilimia 3.62
hawakufanya kutokana na sababu mbalimbali. Akizungumzia ubora wa ufaulu
kulingana na madaraja kwa watahiniwa wa shule, Dk Msonde alisema
watahiniwa 35,880 sawa na asilimia 83.74 wamefaulu daraja la kwanza hadi
la tatu, wasichana wakiwa 12, 108 sawa na asilimia 87.30 na wavulana
23, 772 sawa na asilimia 82.04. Alisema wanafunzi 325 walipata daraja la
kwanza, 5,372 daraja la pili, 30,183 la tatu, 4,362 la nne na 2,604
daraja la sifuri. “Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule unaonesha
kuwa masomo ya Historia, Jiografia, Kiingereza, Kemia, Biolojia, Kilimo,
Sayansi ya Kompyuta, Uchumi na Uhasibu yalifanyika vizuri
ikilinganishwa na mwaka jana,†alisema Dk Msonde. Kumi Bora, Mbaya
Alitaja shule zilizofanya vizuri kwa kundi la watahiniwa zaidi ya 30
kuwa ni Marian (Pwani), Mzumbe (Morogoro), Feza Wavulana (Dar es
Salaam), Ilboru na Kisimiri (Arusha), St Maryâs Mazinde Juu (Tanga),
Tabora Wasichana (Tabora), Igowole (Iringa), Kibaha (Pwani) na Kifungilo
(Tanga). Kundi la shule 10 zilizofanya vibaya ni Pemba Islamic College
(Pemba), Mazizini (Unguja), Bariadi (Simiyu), Hamani, Dunga, Lumumba
(Unguja), Oswald Mangâombe (Mara), Green Acres (Dar), High View
International na Mwanakwerekwe (Unguja). Dk Msonde alisema kundi la
shule zenye watahiniwa chini ya 30, zilizofanya vizuri ni Palloti
Wasichana (Singida), St. James Seminary, Parane, Sangiti (Kilimanjaro),
Itamba (Njombe), Masama Wasichana (Kilimanjaro), Kibara (Mara), St.
Luise Seminary (Morogoro) na Peramiho Wasichana (Ruvuma). Alisema katika
kundi hilo, shule zilizofanya vibaya ni Mbarali Preparatory na Philter
Federal (Unguja), St. Mary na Mzizima (Dar es Salaam), Hijra Seminary
(Dodoma), Tweyambe (Kagera), Mpapa na Al-Falaah Muslim (Unguja),
Presbyterian Seminary (Morogoro) na Nianjema (Pwani). Wanafunzi
‘vichwa’ Akizungumzia watahiniwa waliofanya vizuri katika masomo
bila kujumuisha masomo ya hiari kwa waliosoma Sayansi ni Erasmi Inyanse
(Ilboru-PCM), Maige Majuto (Kisimiri-PCM), Gasper Mungâo (Feza
Wavulana – PCB), Gasper Setus (St. James Seminary-PCM), Lucylight Mallya
(Marian Girls-PCB). Alisema kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwenye
masomo ya Biashara ni Eric Mulogo (Tusiime), Aliacia Filbert (Nganza),
Evart Edward (Kibaha), Annastazia Renatus (Tambaza) na Peterson Meena
(Mbezi Beach). Msonde alitaja waliofanya vizuri kwenye masomo ya Lugha
na Sayansi Jamii kuwa ni Asia Mti (Barbro-Johansson), Godlove Ngowo
(Majengo), Johnson Macha (Njombe), Hamis Mwita (Ilboru) na Sia Sandi
(Marian Wasichana). Matokeo yazuiwa Aidha, Msonde alisema Baraza
limezuia matokeo ya wanafunzi 89 wa shule ambao hawajalipa ada ya
mtihani, wanafunzi 10 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa
kufanya baadhi ya mitihani na 17 kwa kushindwa kufanya mitihani yote
kutokana na ugonjwa. “Wanafunzi hawa 27 tumewapa nafasi ya kufanya
mitihani yao mwakani, wale ambao hawakufanya baadhi ya mitihani
watafanya ile tu ambayo hawakuifanya na 17 ambao hawakufanya kabisa
watafanya wote. Dk Msonde alisema Baraza pia limefutia matokeo wanafunzi
wanne; mmoja akiwa wa shule na watatu wa kujitegemea kutokana na
udanganyifu,alisema.